Fadhili za Mungu na Rehema Zake
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Yoeli 2:12,13 Lakini hata sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.
Maisha huwa na tabia ya kugeuka ghafla kutoka kwenye vipindi vizuri na kwenda kwenye vipindi vibaya; kutoka kuwa chakula kwenda kwenye kipindi cha njaa; kutoka kwenye furaha kwenda kwenye huzuni. Halafu, kadiri mtu anavyozidi kwenda mbali na Mungu, ndivyo matatizo yanavyoongezeka.
Nabii wa Agano la Kale aitwaye Yoeli alitabiri muda kama huo; wakati nzige wanavamia nchi na kukawa na ukame; hali ikawa ngumu mno kwa wateule wa Mungu.
Kwanini hayo yaliwapata? Yalitokana na nini? Mungu mwenyewe anajibu maswali hayo moja kwa moja kupitia nabii wake:
Yoeli 2:12,13 Lakini hata sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.
Taifa teule la Mungu walikuwa wameenda mbali na Mungu kwa sababu ya dhambi zao. Si imekutokea hata wewe, si kweli? Ninakuelewa. Halafu, badala ya kuwaadhibu zaidi, badala kuendelea kuwa mkali na kuwakaripia zaidi, anawaita wamrudie kwa moyo wao wote.
Mkamrudie BWANA Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema.
Kuna wakati, tena ni mara nyingi tu, tukipita ile kona ya njia ya maisha na kwenda mbali na Mungu, tunapata matokeo ya moja kwa moja ya dhambi yetu, Lakini, hata kama Mungu anaruhusu matokeo ya dhambi tulizozifanya kutupata ili tuweze kujirudi, moyo wake – unataka tumrudie, tuwe karibu naye tena.
Mkamrudie BWANA Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.