Hali Inayoleta Ongezeko
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Matendo 9;31 Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
Mtu akifuata vyombo vya habari, ataambiwa kwamba kanisa hua linafifia. Habari hii inawafurahisha makundi mbali mbali ya wapinzani. Lakini hao waandishi wa habari hawatangazi jinsi kanisa linaongezeka sana sehemu nyingi duniani, kwamba linajengwa na kustawi vizuri.
Vipi? Wewe unaonaje? Unafurahi kusikia kwamba watu wanazidi kubadilika kuwa Wakristo, au labda habari hiyo inakutisha kwamba inaturudisha kwenye siku za kale ambazo zilipitwa na wakati? Hailishi uko upande gani, ujue tu kwamba vituo vya mayatima, mahospitali, shule nyingi, vyuo na misaada kwa maskini na waliotengwa – haya yote katika historia, yametokana na jitihada za Wakristo duniani kote.
Sasa ni yapi yanasababisha kanisa moja kustawi na kukua wakati kanisa lingine linadumaa? Sikiliza tena mstari tuliosoma jana:
Matendo 9;31 Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
Katika lugha ya siku hizi, wengine wangesema kwamba kanisa wakati ule lilikuwa na uamsho. Ni vipi vilivyosababisha wakue na kuongezeka? Kwanza, waliishi kwa amani, pili, walimheshimu Mungu na kumtii. Kwa hiyo walipata baraka na waliwezeshwa na Roho yake Mtakatifu.
Kumbe! Inaonekana kwamba uamsho hua unatokea wakati Wakristo wanaanza kutii Neno la Mungu!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.