... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hekima ya Kale (4)

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Tito 2:6,7 Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi; katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu.

Listen to the radio broadcast of

Hekima ya Kale (4)


Download audio file

Kuwa na mke mmoja tu ni mchango mkubwa sana Ukristo ulioweza kuziletea jamii tunazoishi leo.  Kuwawajibisha wanaume kuonyesha upendo, kuhudumia wenzao na kujithibiti na kuwa na kiasi katika swala la mahusiano na wanawake, kwa kweli kumeleta mafao mengi sana.

Ni kweli, mambo hayajatimilika bado kuhusu uhusiano kati ya wanaume na wanawake.  Katika nchi nyingi, wanawake hawalingani na wanaume – kwa malipo na kwa njia nyingine nyingi tu.  Pia, kuna wanaume wengi hawajajifunza kuwa na kiasi, hawajakuwa na hekima ya kuwatendea wanawake kwa upendo na heshima, kama vile Mungu alivyokusudia tangu mwanzo. 

Wiki hii tumepitia mistari inayoeleza namna wazee wanaume na wazee wa kike wanavyopaswa kuwa vielelezo vya kuigwa na kufundisha vijana waume na wanawake namna wanavyopaswa kuishi. 

Tito 2:6,7  Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi; katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu. 

Upende, usipende, kwa kawaida, wanaume wana nguvu kuliko wanawake, kitu kilichosababisha wanawake kuishi kwenye mazingira hatarishi na ya ukatili kwenye karne za awali, – kwa hizuni bado katika sehemu kadhaa na katika ndoa kadhaa za wakati huu kinatumika. 

Kwahiyo, hata kama Maandiko yaliandikwa miaka 2000 iliyopita, kufundisha vijana waume kuwa na hekima bado ni muhimu sana kama ilivyokuwa wakati ule.  Ninyi wazee muwe vielelezo vyao.  Inatakiwa muwafundishe vinana namna wanavyotakiwa kuwatendea wanawake. 

Laiti sisi wanaume wazee, kwa kutumia mifano yetu mizuri, tungeweza kuwafundisha taratibu, vijana wetu kwa upole na kwa uthabiti kuwa wenye busara, waaminifu na wastahivu – tungebadilisha dunia hii kwa kweli!  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly