... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hekima ya Kale (5)

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Tito 2:8 Na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.

Listen to the radio broadcast of

Hekima ya Kale (5)


Download audio file

Mtazamo wa Kikristo kuhusu nafasi za wanaume na za wanawake unadhihakiwa sana siku hizi.  Wanaupinga na kuukosoa kwasababu unaonekana kama hauendani na hali halisi ya karne hii ya 21.

Ukweli ni kwamba Neno la Mungu linafundisha wazi kuhusu kuheshimiana, kupendana na kunyenyekeana kati ya wanaume na wanawake, likitambua pia utofauti wa msingi kati ya roho ya mume na roho ya mke, hali ambayo hakuna mwanasaikolojia stahivu angeleta ubishi … lakini bado wengi hawauoni hata kidogo katika hao wanaokosoa. 

Katika ndoa yangu, kama mume, mimi ni kichwa cha nyumba yetu kama vile Biblia inavyofundisha.  Lakini pia, kama vile Biblia inavyofundisha, ninamhudumia mke wangu, na mimi ninamnyenyekea, sina haki ya kumtawala kimabavu hata kidogo.  

Waefeso 5:25  Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajii yake. 

Nadhani sitakosea endapo nikikukumbusha kwamba Kristo alikufa kwa ajili yetu, na yeye sasa ni kielelezo kwa kila mume katika kila ndoa, ili awe tayari kutoa uhai wake kwa ajili ya mke wake.  Sasa kweli hizi zenye nguvu zikiwekwa kwenye utendaji, zitaleta matunda ambayo wengine hawawezi kuyapuuza. 

Tito 2:8  Na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu. 

Angalia, kuhusu swala hili la mahusiano ya waume na wake, hekima ya dunia hii kwa sehemu kubwa, imetupa yote pale ilipojaribu kuboresha. 

Akina baba na akina mama … kuhusu mahusiano yenu, shikilia sana Neno la Mungu.  Waulimwengu wanaweza kukukosoa, lakini hawataweza kuwa na ya kunena juu yenu wakati watakapoona matunda mema yatokanayo na mahusiano mliyo nayo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly