Kubadilishwa na Neema
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
2 Petro 3:17,18 Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu. Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.
Kuna kipindi kila mzazi anakuwa na hofu kwamba mtoto wake anaweza kuingia katika kundi la wahuni; kwamba wale watu wanaweza kupotosha mwana wake au binti yake. Na kweli ana haki kuhofia hatari kama hiyo.
Mimi binafsi naweza kushuhudia hayo. Wakati watoto wanakua na kuanza kujitafutia maisha, kunatokea mvutano kati ya upendo, elimu na nidhamu waliyopokea nyumbani na mambo mengi yaliyoko “huko” ambayo yanaweza kuwapotosha.
Ni yapi yatakayopata ushindi hatimaye? Ni yale tuliyowafundisha, ule upendo tuliowapenda, ndivyo vitashinda? Hili ni swali kila mzazi anaweza kujiuliza. Na hii inakuwa ishu kwa upande wa Mungu pia, ndiyo maana anasema yafuatayo:
2 Petro 3:17,18 Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu. Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.
A.W. Tozer aliwahi kusema kwamba tusipobadilishwa na neema, inawezekana hatujaokolewa na neema. Naona hakukosea kwa kutamka hivi.
Usipotoshwe. Kua katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.