... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuipinda Injili

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 3:19-21 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Kuipinda Injili


Download audio file

Siku hizi mfuasi wa Yesu yoyote anasongwa sana watu wakijaribu kumlazimisha aipindishe imani yake, abadilishe uelewa wake wa Injili ya Yesu Kristo, utoke kwenye tafsiri ya zamani wanayoosema kwamba ilipitwa na wakati ili uende sambamba na mfumo wa jamii na maadili ya leo.  Kwa kweli tunasongwa mno.

Wakati ule nilipomwamini Yesu, nikaamini Habari Njema kwamba kifo chake kililipa deni la dhambi zangu, kwamba nilisamehewa kupitia mateso yake, nikapata maisha mapya, uzima wa milele kupitia ufufuo wake … hayo yote niliyaelewa sana tena kwa urahisi. Pia, Mungu alisema ni mema, kwa kweli ni mema.  Na yale aliyoyasema kuwa maovu yalikuwa maovu, basi.  Hapakuwa majadiliano. 

Lakini baada ya muda, niligundua kwamba wale ambao hawamwamini Yesu, hawakupendezwa na mtazamo wangu rahisi. Yaani kulikuwa na vipengele katika mtazamo wangu ambavyo viliwakwaza mno.  Kwahiyo nilianza kusongwa ili niafikiane nao kwa swala hilii linalohusu ukweli; nipindishe Injili ili niwapendeze angalau nikubaliane na dhambi zao. 

Lakini kama vile Yesu mwenyewe alivyoeleza kuhusu watu hawa … 

Yohana 3:19-21  Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.  Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.  Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu. 

Tafadhali tukubaliane hapo. Yesu alipokaa na wenye dhambi, wao ndio waliobadilika, sio yeye.  Kwahiyo, usiipindishe Injili. Usitie giza kwenye nuru yako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.