... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kumpendeza Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 14:6-10 Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode. Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lo lote atakaloliomba. Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe; akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani.

Listen to the radio broadcast of

Kumpendeza Mungu

Download audio file

Tumaini letu tulilo nalo sirini ni kwamba tukimfuata Yesu, tukimtii basi atatubariki. Afya njema, mali na hekima. Hilo ni tumaini.

Lakini kwenye kiini cha moyo, kwamba yawezekana haitakuwa kama tulivyotazamia; kwamba hata hivyo mabaya yatatupata na jitihada zetu katika kumfuata Yesu zitakuwa kazi bure. Yaani kumfuata Yesu ni kujihatarisha na hasa kutazamia thawabu kutoka kwake. Lakini wewe na mimi, tunajua kwamba mabaya huwa yanatokea.  Kuna wengine, kama vile Yohana Mbatizaji, walipata mateso makubwa hata kama walitenda mema siku zote. 

Mathayo 14:6-10  Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode.  Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lo lote atakaloliomba.  Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.  Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe; akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani. 

Yohana Mbatizaji alimtii Mungu kabisa lakini bado Mungu aliruhusu akatwe kichwa.  Kwahiyo jibu linapatikana wapi?  Jibu halitapatikani kwenye mapambo ya dunia hii, hapana.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.