Kumpendeza Roho
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Wagalatia 6:8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Je! Naweza kukuomba leo uvute pumzi vizuri na kujiuliza swala hili: Je! Ninaishije maisha yangu? Ni kweli, maisha yana makona mengi tena yanasumbua. Lakini katikati ya misukosuko yote, je! Unaishije? Au tutumie mfano huu kwa kuuliza, je! Umepanda mbegu gani kwa ajili ya maisha yako ya baadaye?
Kwa hiyo, tumfikirie mkulima fulani anayelima shamba lake na kupanda mbegu za mahindi kwa muda mwafaka. Hali ya hewa inamkubalia, mambo ni sawa, kwa hiyo anaenda kujishughulisha na mambo mengine, akisahau ni aina gani ya mbegu aliyopanda shambani mwake.
Wakati vichipukizi vinaanza kuonekana kutoka ardhi, anaanza kuwa na mashaka kwamba mambo si sawa. “Je! Sikupanda ngano shambani mwangu?” Lakini kadiri siku zinazoenda, matazamio yake kwamba atavuna ngano yanafifia na anakatishwa tamaa kuona kwamba atavuna mahindi.
Najua kwamba wengine watacheka kusikia mfano huu kwa sababu haieleweki. Je! Kuna mkulima ataweza kudanganyika hivyo asijue mbegu aliyepanda? Ni kweli, lakini hata hivi, ukiangalia jinsi watu wanavyoishi, wengi wao wakijaribu kutimiza tamaa zao binafsi lakini bado wanatazamia kuvuna uzima wa milele ambao haupo kwa ajili yao, hautashangaa tena.
Wagalatia 6:8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Rafiki yangu, kumpendeza Mungu, kumtii, na kutembea katika Roho yake, kumwamini Yesu na kuishi kama vile kweli unamtegemea Yesu, hii ndiyo njia ya uzima wa milele. Hii ndiyo njia ya kuvuna mavuno uliyotazamia. Lakini Yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu.
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.