... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuna Njia Moja Tu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Timotheo 2:5,6 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.

Listen to the radio broadcast of

Kuna Njia Moja Tu


Download audio file

Kwanini mfumo wa jamii siku hizi uko kinyume kabisa na Ukristo?  Ni yapi yamewafanya watu wengi kukwazika hivi na Habari Njema za Yesu?  Kuudhiwa unaongezeka kwa kweli, ni kwa nini?

Siku zilizopita nilishiriki kipindi cha kujadili Biblia kwenye kundi ndogo lenye watu wa tabaka mbalimbali na maoni tofauti-tofauti. 

Kulikuwa na mtu mmoja aliyeamini kwamba Biblia ni kama alama zinazoweza kuwaongoza watu kwa Mungu. Yeye alikuwa ametafiti imani ya Buddha pamoja na kusoma Kurani.  Alitafiti pia imani zingine huku akitoa hela nyingi kununua vitabu na CD kutoka kwa walimu na viongozi mbalimbali. 

Tulikuwa tunajifunza Injili ya Yohana wakati ule, sasa maoni yake yalikuwa ni kwamba kitabu, kitabu cha Yohana kilikuwa kinaainisha mambo tu, Yesu asingeliweza kubadilisha maji kuwa divai.  Na pale Yesu aliposema kwamba, “Mimi ndimi njia, na kweli na uzima.  Hakuna awezaye kufika kwa Baba bila kupita kwangu.” … mtu yule alisema kwamba mwandishi alijidanganya tu.  Kwa maoni yake, yeye anafikiri kuna njia nyingi tu kufika kwa Mungu.  Lakini Mungu mwenyewe hajasema hivi. 

1 Timotheo 2:5,6  Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake. 

Kule kukana ukweli hakujaufanya ukweli kuwa uongo.  Kujitolea kwa Yesu pale msalabani ndiko kulikoweza kulipa gharama ya dhambi zako na zangu.  Kifo chake na kufufuka kwake vinafungua mlango wa kuingia na kupata mahusiano na Mungu yatakayoendelea milele.  Kuna njia moja tu.  Yesu.  Huu ndio ukweli na hakuna mwingine.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.