... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuondoa Doa ya Dhambi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Listen to the radio broadcast of

Kuondoa Doa ya Dhambi


Download audio file

Unapotenda jambo unalojua kuwa ni baya, ukweli wa dhambi ile unaendelea kama doa ya damu kwenye kitambaa cheupe.  Inaonekana kuwa haliwezi kutoka, kwa hiyo hatia inakutafuna nafsini mwako kama kansa.

Ni muhtasari wenye masikitiko, lakini si jambo jipya.  Katika tamthilia maarufu ya Shakekspeare, Bibi Macbeth, akisumbuliwa na hatia ya mauaji, anaangalia mikono yake iliyochafuliwa na damu; na kupiga yowe, “Toka we doa uliyelaaniwa, nasema, Toka! 

Nia hiyo ya dhambi kuondolewa, ubaya kutatuliwa, hatia kufutwa, ni sehemu ya hali ya kibinadamu kote duninai.  Hali hii ilisababisha Mungu achukue hatua kali ya kuruhusu Mwanae asulubiwe kwa niaba yetu. 

Je! Tunaweza kuepushwa na dhambi zetu kabisa?  Je! Tunaweza kuwekwa huru kweli kweli na hatia inayotutafuna hata ndani ya mifupa yetu?  Au tuko kama Bibi Macbeth, aliyeandikiwa kuishi katika majuto ya matokeo ya dhambi yake milele yote? 

Sikiliza leo anavyosema Mungu kuhusu tatizo hili linalogusa suala la uzima na mauti: 

Isaya 1:18  Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA.  Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. 

Kuna sehemu moja – ni moja tu – ambapo doaya dhambi inaweza kuondolewa.  Kuna mtu mmoja – ni mmoja tu – anaweza kuosha dhambi zako.  Ni Yesu, Mwana wa Mungu, aliyekufa alipe deni la dhambi zako.  Sasa, mtu akimwamini, dhambi zake zote zinasamehewa.  Zinasamehewa kabisa. 

Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.  

Ni ndani ya Kristo peke yake. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.