ni Afadhali Kuteswa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
1 Petro 3:17 Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya.
Kuteswa ni mada ambayo ninapenda kuirudia mara kwa mara, nataka nielemishwe zaidi na kupiga hatua mbeleni na ninatarajia kwamba inaweza kukusaidia pia katika hatua hizo. Ni kwa sababu tunapopata mateso, ndipo tunapoweza kupata fursa kubwa kuliko zote Mungu anazotukirimia.
Mwanariadha yoyotee atakwambia kwamba anateswa sana wakati wa mazoezi. Ili mtu ajenge misuri, ni lazima aumie. Kujifunza kustahimili inaumiza. Lakini kwa wanariadha ni mateso yenye malengo maalum. Ni mateso kwa ajili ya kuboresha ujuzi na ustadi wao katika michezo ili waweze kuwa wepesi zaidi. Ndio maana wanakubali kujitesa.
Na hivyo ndivyo ilivyo katika maisha yetu pia. Tunajua kwamba vipindi vigumu ndivyo Mungu huwa anavitumia kufinyanga tabia zetu vizuri; akitufundisha kumtegemea zaidi. Ni kipindi kizuri cha kutulainisha na kututengeneza ili tuweze kufanana zaidi na Yesu.
Lakini – kwa nini kuna “walakini siku zote? – mara nyingi mateso yanatokana na uonevu na kule kuonewa kunasabasha kiburi chetu kipande. Yaani, kunyimwa haki kunatupa mtazamo mbaya unaoweza kuzuia mafao yale Mungu aliyotaka kuingiza katika tabia yetu kupitia mateso yale. Daima, kiburi kinazuia baraka za Mungu, si kweli?
Kwa hiyo, hii ikitokea maishani mwako, basi sikiliza vizuri:
1 Petro 3:17 Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya.
Petro aliandikia maneno haya kwa Wakristo waliokuwa wanateswa vibaya na kunyimwa haki zao kwasababu ya imani zao ndani ya Yesu. Kama Mungu anaruhusu kipindi cha mateso kikujie, na kama ni mapenzi yake, basi yapokee kwa furaha. Uteswe na moyo mweupe na kwa mtazamo mwema hata kama inaonekana kwamba umeonewa sana … kwa sababu Mungu anakuandalia kitu kizuri sana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.