... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Je!, Umechoka?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Isaya 40:30,31 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

Listen to the radio broadcast of

Je!, Umechoka?


Download audio file

Sisi sote tunaweza kuchoka mara kwa mara.  Haijalishi una nguvu kiasi gani wala juhudi zile ulizo nazo kwa kawaida, tutafika mahala ambapo mambo yatatuzidi.  “Je! Nina tatizo gani, mbona nimechoka mno?”

Mimi mwenyewe nilipitia kipindi kama hicho miezi michache iliyopita, nilichoka sana hadi nikaishiwa nguvu kabisa.  Yaana uchangamfu wangu wa kawaida ulikuwa umetoweka. Si kwamba mambo maishani mwangu yalikuwa magumu, hapana, ni kama juhudi yangu ilikuwa imetoweka tu. 

Kwahiyo, nilitaka uelewe kwamba kuishiwa nguvu si wewe tu. Hata sisi huwa inatutokea mara kwa mara. Inapotokea sasa huwa tunatafuta jibu lakutusaidia: Labda nahitaji likizo, au labda nitafute ajira sehemu nyingine, ni mara chache tunatafuta jibu sahihi mahala panapofaa. 

Isaya 40:30,31  Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. 

Unaona?, Kuishiwa nguvu kabisa huko kunawapata hata wenye nguvu kuliko wengine: vijana, Sasa hata tukipata likizo ya siku nyingi, mapumziko au cho chote ambacho dunia hii inaweza kutupatia, yote haya hayatatatua tatizo hilo.  Jibu ni Kumgojea Bwana. 

Na neno hilo hapa lina maana kwamba mtu anangoja akiwa na matazamio; kusubiri akiwa na imani; kungoja kwa kutazamia yale Mungu atakayoyafanya.  Tulia na umngoje yeye … na hapo utarudishiwa nguvu.  Utapanda juu kwa mbawa kama tai.  Utapiga mbio, wala hutachoka. Utakwenda kwa miguu, wala hutazimia. 

Subiri ukiwa na matazamio. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.