... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uwe Hodari

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 4:14-16 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi natukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri,ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Listen to the radio broadcast of

Uwe Hodari

Download audio file

Achani kuulize, je!  Unatazamia nini kwa maisha yako ya baadaye?  Naamini kwamba unayo mipango mizuri kwa ajili ya mwaka huu ambao tumeuanza hivi karibuni.  Sisi sote tunayo mipango.  Lakini inawezekana kwamba kuna mawingu meusi yanayo kusanyika na kukuletea mashaka pia, ukianza kufadhaika kuhusu jinsi itakavyokuwa huko mbeleni.

Kama umeshasoma habari ya maisha ya Yesu na huduma yake katika Injili ya Mathayo, Marko, Luka na Yohana, bila shaka kama vile mimi, umeshangaa mno kusoma habari za miujiza yake ya ajabu, kufundisha kwake kwenye nguvu, kifo chake na ufufuo wake. 

Lakini je!  Umewahi kufikiri mambo kwa mtazamo wake?  Alikutana na matatizo, mengitu. Alikumbana na vipingamizi kutoka kwa Ibilisi na mapepo wake, hata kutoka kwa viongozi wa dini … na hata kutoka kwa umati wa watu walio shuhudia uwezo wa miujiza yake.  Hayo yote ndiyo sababu mtu anaweza kumtegemea kuhusu maisha yake ya baadaye. 

Waebrania 4:14-16 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.  Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.  Basi natukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri,ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Yesu alipitia hayo yote – kila jaribu, kila kipingamizi ambavyo wewe na mimi tungeweza kukumbana navyo, hata zaidi.  Kwa hiyo anatuelewa vizuri kabisa.  Kwa sababu hiyo – wewe na mimi, tunaweza kuja mbele za kiti chake cha enzi kwa ujasiri ili tupate rehema yake na kugundua neema yake muda ule ule wa mahitaji yetu.  Unaweza kumtegemea Yesu na kumkabidhi hatima yako.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.