... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuirudisha Nuru ya Imani Yako Kama Vile Katika Kioo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wakorintho 3:17,18 Basi “Bwana” ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukutu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.

Listen to the radio broadcast of

Kuirudisha Nuru ya Imani Yako Kama Vile Katika Kioo


Download audio file

Imani yetu,.. yako na yangu, haiwezi kuwepo nje ya mazingira yetu wala nje ya umma na yote yanayoendelea mahali tulipo.  Hata kidogo.  Imani ilikusudiwa kuwa sehemu ya maisha ya kila siku … na hii ndiyo inatuletea changamoto kabisa.

Swali ambalo latupasa sisi sote kujiuliza mara kwa mara:  Je!  Imani yangu inadhihirisha hasa utamaduni wetu, maoni yangu ya siasa, hali yangu ya uchumi au imani yangu inamdhihirisha Yesu ulimwenguni? Ina maana, ni kipi kinachotangulizwa?

Wengi wanatanguliza vitu kinyume kabisa, yaani imani ya Wakristo wengi inaundwa zaidi na siasa na swala la pesa kuliko jinsi tungependa kukiri.  Wewe unaonaje?  Wakati bado unatafakari, ebu nikuonyeshe jinsi inavyotakiwa itendeke:

2 Wakorintho 3:17,18  Basi “Bwana” ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.  Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukutu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.

Kwa maneno mengine, badala ya kufananishwa na mfumo wa jamii wa kisasa na maporomoko ya maadili yanayoendana na mfumo huo, sisi tunabidi kubadilishwa na kufananishwa na Mungu, tukizidi kuwa kama alivyo yeye.  Kinachohuzunisha sasa ni kwamba maisha ya Wakristo wengi yanaenda kinyume kabisa na kusudio hilo.

Ikitokea kama inavyotakiwa, utukufu wa Mungu ungezidi kudhihirika kutoka imani yetu kama vile kioo inavyorudisha nuru, badala ya kuigushi imani yetu na mambo yaliyopo duniani.  Tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo.

Ilitakiwa itendeke hivyo na … 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.