... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ni Yapi Yaliyo Mema?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mika 6:8 Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!

Listen to the radio broadcast of

Ni Yapi Yaliyo Mema?


Download audio file

Tunaishi katika ulimwengu wenye utofautishaji kabisa.  Weusi na weupe.  Warefu na wafupi.  Matajiri na maskini.  Vijana na wazee.  Lakini kilicho muhimu kuliko vyote ni hiki: mema na mabaya.  Kwa hiyo, tuulize, je!  Kuna utofauti gani kati ya mema na mabaya?

Kwa kweli, kadiri maadili yanavyoporomoka, ndipo inazidi kuwa vigumu kutenganisha mema na mabaya ,wakati huu watu ambao bado wanaoishikilia dhana ya mema na mabaya wanadhihakiwa hata kuteswa.

Kama vile Mtume Paulo aliweza kusema baada ya kuchunguza mambo (Warumi 1:32), si kwamba jamii imeharibika kiasi cha kuruhusu watu kutenda maovu bila matokeo, bali imefika mahala pa kuyakubali na kuyapongeza na kuwatia moyo wanaoyatenda.

Sawa, najua hayo yaliyoandikwa miaka elfu mbili iliyopita, lakini leo hali hiyo imezidi kabisa.  Wanaotenda maovu na kuyakuza wanataka kufuta utofauti, wakichanganya rangi nyeusi na rangi nyeupe kupata aina hamsini ya rangi ya kijivu … hadi pale watu wengine hawajui “mema” yanafananaje.  Sasa tuulize, je!  “Mema” hua yanafananaje?

Mika 6:8  Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!

Kipindi hiki wakati tunaambiwa kwamba hakuna uhakika katika swala la maadili, kwamba umeshpitwa na wakati, wakati tunashawishika sana tukubali kanuni potovu ambazo wengi wanaona sasa kuwa kawaida … inabidi tusimame, tumsikilize Mungu halafu tutende mema.

Yaliyo mema ni yapi? 

BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.