... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tuendelee Hadu Tufikie Makuu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 71:20,21 Wewe, uliyetuonyesha mateso mengi, mabaya, utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena tokea pande za chini ya nchi. Laiti ungeniongezea ukuu! Urejee tena na kunifariji moyo.

Listen to the radio broadcast of

Tuendelee Hadu Tufikie Makuu


Download audio file

Mateso yakikupata, je!  Umejiuliza kama Mungu mwenyewe alisababisha yatokee?  Je!  Msiba ule uliweza kupenyeza bila yeye kujua au daima ulikuwa sehemu ya mpango wake?  Na kama ilikuwa mpango wake, je!  Alikuwa anafikiria nini?

Mimi binafsi nimewahi kujiuliza swali hilo mara nyingi kwa sababu wakati shida inanijia, ninaanza kukwazika na kuanguka na kujiuliza … Je!  Hii ni nini?!  Ndiyo maana mtu anaanza kuuliza maswali magumu. 

Jana tulikuwa na masimulizi kwamba Mungu anaeleza habari ya uaminifu wake usiokoma pamoja na fadhili zake mara ma-mia ndani ya Biblia.  Kwa nini?  Kwa sababu hua inachukua muda mrefu na matukio mengi ili ukweli wa uaminifu wake na upendo wake kutuingia kabisa na kuwa sehemu ya maisha yetu ili wakati wa mateso, tuwe na amani tukijua kwamba kamwe hawezi kutuacha wala kutupungukia. 

Sasa, ile kazi endelevu Mungu anayoifanya ndani ya kila mmoja wetu, ndiyo mada ya mtunga Zaburi wakati alitamka hivi akimwambia Mungu: 

Zaburi 71:20,21  Wewe, uliyetuonyesha mateso mengi, mabaya, utatuhuisha tena.  Utatupandisha juu tena tokea pande za chini ya nchi.  Laiti ungeniongezea ukuu!  Urejee tena na kunifariji moyo. 

Anafahamu kwamba Mungu anatamalaki juu ya mateso yake na vipindi vigumu anavyopitia.  Anakiri kwamba Mungu ndiye aliyeruhusu yampate.  Lakini katikati ya majaribu hayo, bado ana moyo mkuu akijua kwamba Mungu atamrejesha na kumwinua tena.  Ndiyo maana alithubutu kusema … Utanihuisha tena.  Utanipandisha juu tena tokea pande za chini ya nchi.  Laiti ungeniongezea ukuu!  Urejee tena na kunifariji moyo.  

Wakati wa shida, umruhusu Mungu akutie moyo uwe thabiti.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.