... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Huzuni Yako Itageuka Kuwa Furaha

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 16:19,20 Yesu alifahamu ya kwamba wanataka kumwuliza, akawaambia, Ndilo hilo mnaloulizana, ya kuwa nalisema, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.

Listen to the radio broadcast of

Huzuni Yako Itageuka Kuwa Furaha


Download audio file

Mungu ni bingwa wa kubadilisha misiba yetu mikubwa imletee ushindi mkubwa.  Hakuna msiba mkubwa katika historia kuliko kuona maiti ya Yesu ilivyotundikwa pale msalabani.

Je!  Msiba mkubwa kuliko yote uliyoupata ni upi?  Tukio lile ambalo kidogo tu, lingekupasua kabisa?  Yamkini bado uko katikati ya msiba ule muda huu huu.  Endelea kushikilia wazo hilo wakati tunachunguza msiba mkubwa kuliko yote iliyowahi kutokea: 

Yohana 16:19,20  Yesu alifahamu ya kwamba wanataka kumwuliza, akawaambia, Ndilo hilo mnaloulizana, ya kuwa nalisema, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona?  Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 

Njama ya kumwamgamiza Yesu ilikuwa imeshawahofisha mno wanafunzi wake.  Waliogopa kwamba mpendwa wao Yesu angesulubiwa lakini pia walihofia uhai wao kwamba na wao wangesulibishwa. 

Halafu, wakati Yesu aliuawa, bila shaka unaweza kufikiria jinsi walijisikia kwamba wameachwa.  Walilia machozi.  Kama vile wewe na mimi tumelia wakati wa msiba mara kwa mara kupitia miaka ya maisha yetu. 

Lakini yule aliyekaribia kutundikwa na misumari pale msalabani, ndiye aliyetamka maneno ya kutuliza machozi yao, machozi yetu … na machozi yako: 

Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.