... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ahadi Kubwa Sana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 14:12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

Listen to the radio broadcast of

Ahadi Kubwa Sana


Download audio file

Yesu alitamka maneno ya kushangaza, maneno yasiyotazamiwa.  Kila wakati mtu anasoma habari zake katika Injili, hawezi kukosa kumshangaa.

Siku hizi chache tumeona jinsi wanafunzi wa Yesu, wale waliokuwa karibu naye, jinsi walimwangusha wakati alikaribia kwenda kusulubishwa.  Kwa kweli walikuwa na moyo mkuu wakati alikuwa anaponya wagonjwa na kutembea juu ya maji na kuhubiri kwa nguvu.

Lakini wakati njama za kumwangamiza zilianza kuvuma, walianza kuhofia uhai wao.  Sasa, wakati Yesu alihukumiwa mbele ya Pontio Pilato, walikuwa wapi?  Walikuwa wamekimbia na kujificha.  Petro aliahidi kwamba atamtetea Yesu mpaka mwisho, lakini kumbe!  Swali la binti mdogo pale akiota moto lilisababisha amkane Yesu mara tatu.

Lakini Yesu alijua vema jinsi watamwangusha, lakini hata hivi, aliweza kuwaambia jamaa hawa ambao walikuwa rafiki wakati wa neema tu, watu wasiotegemewa, aliwaambia kwamba:

Yohana 14:12  Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

Hakutazama dhambi zao.  Yeye alijua watakavyoshindwa.  Lakini bado alikuwa na mpango.  Mpango wa kufanya wahesabiwe haki mbele za Mungu  akilipa deni la dhambi zao pale msalabani.  Mpango wa kuwabariki kuliko ambavyo wangefikiria.  Mpango wa kutumika kwa nguvu kupitia wao, ili maisha yao yatikise watu ma-biliyoni kupitia hii miaka elfu mbili na kuendelea.

Na sisi tunafeli kama wao.  Dhambi yao ni ya kwetu pia.  Hatuko tofauti!  Kwa hiyo, ukijiangalia kwenye kioo na kuona dhambi yako tu, kumbuka hili, Yesu anao mpango.  Habari njema inakuja!  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.