... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Licha ya Kusudio Lako Bora

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 13:36-38 Simoni Petro akamwambia, Bwana, unakwendapi? Yesu akamjibu, Niendako huwezi kunifuata sasa; lakini utanifuata baadaye. Petro akamwambia, Bwana, kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa? Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako. Yesu akamjibu, Je! Wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia, Jimbi hatawika hata wewe utakapokuwa umenikana mara tatu.

Listen to the radio broadcast of

Licha ya Kusudio Lako Bora

Download audio file

Ni vizuri kuwa na makusudio mema, lakini kuyatekeleza ni swala lingine kabisa.  Hakuna mwanadamu anayeishi leo ambaye hakuanza safari akiwa na malengo mazuri, lakini akajikwaa mapema tu.

Siku zilizokaribia Pasaka, njama za kumwangamiza Yesu zilikuwa zimewiva kabisa.  Wanafunzi walikuwa na hofu kuu wakati waliona viongozi wa dini walikuwa wanazingira wakishirikiana na wakoloni Warumi.  Hata Yesu mwenyewe alikuwa amewaambia kwamba anakaribia kuondoka.

Yohana 13:36-38  Simoni Petro akamwambia, Bwana, unakwendapi?  Yesu akamjibu, Niendako huwezi kunifuata sasa; lakini utanifuata baadaye.  Petro akamwambia, Bwana, kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa?  Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako.  Yesu akamjibu, Je!  Wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu?  Amin, amin, nakuambia, Jimbi hatawika hata wewe utakapokuwa umenikana mara tatu.

Petro alikuwa na nia njema kabisa, amtetee Yesu mpaka mwisho.  Nadhani unafahamu yaliyofuata.  Alifeli kabisa.  Hayo tutayaangalia kesho.

Yamkini unaweza kumwelewa vizuri.  Na wewe ulikuwa na makusudi mazuri sana ya kumfuata Yesu, lakini wakati mambo yaliyokuwia vigumu, wakati ulikutana na wapinzani, kumbe!  Uligundua kwamba pale alipoenda Yesu ulishindwa kumfuata.

Sasa hatia pamoja na hisia kwamba hufai kwa kuwa umeshindwa zinazidi kukuumiza hasa ukikumbuka nia njema uliyokuwa nayo mwanzoni.  Lakini usikate tamaa.  Kuna habari njema inayokuja, rafiki yangu.  Habari njema inakuja.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.