... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tafsiri Halisi ya Kushindwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 12:20,21 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Tafsiri Halisi ya Kushindwa


Download audio file

Je!  Umewahi kujitahidi sana na kujinyima mengi ili uweze kutimiza lengo fulani halafu ukishafanikisha, unakuta kwamba kumbe, bado kuna pengo, bado hujaridhika, kwamba mafaniko hayakuwa kama uliyoyatazamia?

Mimi mwenyewe ninaelewa hisia hiyo ya ubatili.  Sehemu ya kwamba ya maisha yangu nilikuwa na shauku kuwa tajiri maarufu.  Kwa kweli nilikuwa nimeanza kupiga hatua – niliendesha gari la fahari, nikiishi ndani ya nyumba ya fahari, nikawa na sifa njema katika fani yangu.  Lakini pengo bado lililokuwepo moyoni liliniumiza mno.

Nikiangalia nyuma, mimi ninaona kwamba tafsiri halisi ya kufeli ni kufanikisha mambo ambayo hayana maana.  Na hii ndiyo mada ya Yesu katika mstari wa tajiri mpumbavu.

Yaani, mashamba ya huyu jamaa yalizaa sana kiasi ilimbidi avunje ghala zake, ajenge kubwa zaidi ili apate pa kuweka mavuno yake.  Sasa, kwa msingi wa mafanikio yake makubwa, alifikia maamuzi kama wengine wengi wanavyofanya na kujiambia, Nimeweka akiba kutosha miaka mingi.  Pumzika, ule, unywe, ufurahie maisha!

Luka 12:20,21  Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako!  Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?  Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.

Mpumbavu we!  Alihodhi mali yake, lakini kumbe hakuelewa kwamba muda umemwishia kabisa!  Hii ni changamoto kwa kila mmoja wetu.

Je!  Nawezaje kuzidi kuwa mkarimu?  Je!  Nawezaje kuzidi kupanda mbegu kwa ajili ya ufalme wake Mungu?

Hayo ni maswali magumu, lakini Yesu aliweka bayana kwamba yule atakayefika mwisho wa maisha yake akiwa bado na akiba ya hela nyingi kwenye akaunti yake benki … hawezi kabisa kuhesabiwa kuwa mshindi, wala! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.