... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kushiba Mahali Pasipokuwa na Maji

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Isaya 58:11 Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.

Listen to the radio broadcast of

Kushiba Mahali Pasipokuwa na Maji


Download audio file

Sisi sote tuna shauku kubwa kuridhika na nafasi yetu katika maisha haya; yaani kutoshelezeka vipindi vizuri na vipindi vibaya pia. Kuwa na amani inayodumu kupitia hatua zote za maisha yetu.

Kinachohuzunisha ni kwamba mara nyingi tunatafuta kuridhika na kutoshelezeka na kupata amani mahali ambapo hapafai kabisa, hivyo tunajiletea wenyewe uharibifu. Hata kama huyu mwanasaikolojia aliyeishi karne iliyopita, Carl Jung hakumwamini Yesu, aliweza kudokeza kinachosababisha watu waharibikiwa kichwani wakitafuta kuridhika: 

Mtu anakuwa mwenye fadhaa palei anaporidhika na majibu yasiyotosha au yasiyo sahihi kwa maswali ya msingi wa maisha. Anatafuta cheo, kufunga ndoa, sifa za watu wengine, mafanikio katika uchumi lakini bado hafurahii na anaendelea kufadhaika hata baada ya kufikia yale aliyokuwa anayatafuta. 

Nadhani sisi sote tumewahi kutafuta sana kuridhishwa na mambo yasiyo sahihi na kukuta kwamba majibu tuliyoyapata hayawezi kuridhisha hata kidogo.  Mfalme wa Israeli, Sulemani alidokeza tatizo hilo hilo miaka elfu tatu iliyopita: 

Mhubiri 5:10,11  Apendaye fedha hatashiba fedha, wala apendaye wingi hatashiba nyongeza.  Hayo pia ni ubatili.  Mali yakiongezeka, hao walao nao waongezeka na mwenyewe hufaidiwa nini, ila kuyatazama kwa macho yake tu?   

Ukweli ni kwamba vitu vya dunia hii haviwezi kuridhisha kweli kweli.  Tunahitaji kitu kidumucho, kitu kinachoendelea katika kila hatua ya maisha. 

Isaya 58:11  Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui. 

Jamani!, Ni mfano mzuri sana! Mungu ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji hadi utakapokuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui. Yeye mwenyewe ndiye jibu, jibu pekee la maswali ya msingi yahusuyo maisha yetu na yeye ndiye awezaye kukuridhisha, utoshelezeke na kuwa na amani endelevu uliyokuwa unaitafuta.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.