... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Makosa Wamama Wanayofanya (2)

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 21:19; 27:15 Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi ... Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, na mwanamke mgomvi ni sawasawa.

Listen to the radio broadcast of

Makosa Wamama Wanayofanya (2)


Download audio file

Mwanamke mgomvi ni kitu kilichochakaa kisichopendeza ingawa wanawake wengi wanachukia na kupinga kwamba si kweli. Ni sawa, wana haki kusema hivyo. Lakini hata hivyo, bado kuna akina mama wagomvi wanaowachokoza wanaume zao, na hivyo, kuathiri ndoa zao.

Angalia, kama mwanaume atasema kwamba atatimiza jambo fulani, atalitimiza.  Hakuna sababu ya kumkumbusha kila baada ya miezi sita!!!  Ni kweli, sisi wanaume tunaweza kusumbua kweli. Ni mara ngapi mke amemwambia mume wake kufanya kitu na hakifanyi, au kutokufanya kitu halafu anakifanya!

Lakini ninyi wake nisikilizeni – kuna hatari. Usimwone mume wako kama mtu aliyevunjika! Hapo ndipo ugomvi unapoanzia. Kadiri mke anavyozidi kumchokoza mume wake, ndivyo mume naye atazidi kumpuuza.

Mithali 21:19  Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.   

Sasa bila shaka, wake wengine watachukia na kulalamika, “Hayo Maneno lazima yatakuwa yaliandikwa na mwanamume!”, madai hayo ni ya kweli.  Kuwa mgomvi na kumchokoza mume haitasaidia mke hata kidogo, kwasababu inamkosesha raha.

Mithali 27:15  Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, na mwanamke mgomvi ni sawasawa.

Ndiyo, na hayo pia yaliandikwa na mwanamume – Hongera Mfalme Suleimani,  uliyekuwa mwenye busara kabisa! Lakini tukiacha utani, kuna mambo mke hataweza kuyabadilisha kwenye tabia ya mumewe (na siwezi kuacha kusema, hata mume hawezi kubadilisha tabia ya mke wake).  Lakini kuchokozana na kugombana kunavunja ndoa nyingi.

Kwahiyo, wewe mke, je! Huwezi kumpenda mume wako jinsi alivyo pamoja na mapungufu yake yote, au utaendelea kuwa mgomvi kwake na kumchokoza hadi uvunje ndoa yako?

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.