... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Shauku ya Kubadilishwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 12:11 Kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana.

Listen to the radio broadcast of

Shauku ya Kubadilishwa


Download audio file

Kila mtu anatamani kuwa na maisha bora – kwa tafsiri yake  anayoijua yeye.  Lakini kwa watu wengi, kumekosekana kitu cha kizembea kinachosababisha wasipate kuishi maisha bora.

Kwa hiyo, Unaishi “maisha bora”? Je!, Uko sehemu Mungu aliyokusudia uwepo, ukijaa furaha na kurudhika hata kama unakutana na vikwazo na visiki njiani?  Au ukitafakari na kuwa muwazi, je! Utakiri kwamba maisha yako yanapungukiwa na hali hiyo bora uliyotarajia?

Na kama kweli unataka kuishi maisha yale, swali linalofuata ni kujua shauku uliyo nayo ya kuyapata.  Je!  Unatamani kweli kweli kuishi maisha tele; kuwa na uzima tele Yesu aliokuja ili aukupe uweze kuzaa matunda mengi kutokana na jitihada zako?

Kuna sababu ninakuuliza maswali hayo – na kweli, ninaelewa kwamba labda yanaweza kuwa maswali yanayosumbua nikichunguza kwa undani – lakini ni kwamba kama huridhiki na maisha yako yalivyo, na kama kweli unataka kuishi maisha yale Mungu alikusudia kwa ajili yako, yamkini hiki ndicho kinachopungua kwako:

Warumi 12:11  Kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana.   

Kuna watu walegevu – yaani kwa lugha ya asili ya Kigiriki ina maana kuwa “mvivu”, ambayo ni kinyume kabisa na mtu mwenye juhudi (mwepesi, mwenye shauku, mwenye bidii).

Nikisema wazi, kuna watu wanatamani kuwa na maisha bora na kumtumikia Bwana, lakini hawana shauku ya kutosha.  Je! Unamfahamu watu kama hawa.Uwe na shauku, uwe na bidii, uwe na juhudi, anza kazi.  Mungu anakusubiri akupe maisha yanayozidi matazamio yako yote.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.