... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usijilipize Kisasi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mambo ya Walawi 19:17,18 Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake. Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi BWANA.

Listen to the radio broadcast of

Usijilipize Kisasi


Download audio file

Mtu akikasirika, na kuona jinsi alivyoonewa na mtu mwingine, ndipo dhana ya kulipiza kisasi inakuwa tamu kwake.

Mgogoro hauna budi kutokea.  Hua unatokea katika familia.  Unatokea katika jamii – je!  Ni mara ngapi majirani wamegombania mipaka?!  Hua inatokea kazini na kanisani … unatokea kote kote.  Watu wana mitazamo tofauti, ghafla mzozo unaanza.  Mmoja anamdhulumu mwenzake, tayari ugomvi unaanza. 

Na kama nilivyosema, ikitokea, muda ule ule dhana ya kufanya kisasi inakuwa tamu kabisa.  Jana tuliongea habari ya amri ya Yesu ya kusamehe wanaotukosa:

Luka 13:3,4  Kama ndugu yako akikosa mwonye; akitubu msamehe.  Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe. 

Leo, tusikilize tena jinsi Mungu anaongea kuhusu mazingira hayo ya migogoro: 

Mambo ya Walawi 19:17,18  Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake.  Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako;  Mimi ndimi BWANA. 

Chuki imefutwa, ni wazi.  Lakini kwa vyo vyote, inabidi kumwonya hata kumkemea jirani ambaye mnazozana.  Lakini hata ikihusu jambo gani, Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo.  Yote mawili ni mabaya.  Sasa badala ya hayo, wakati unajaribiwa ulipize kisasi, muda ule ule (sikiliza vizuri!) … umpende jirani yako kama nafsi yako.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.