... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uwezo wa Kushinda Hofu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Timotheo 1:5-7 Nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo. Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

Listen to the radio broadcast of

Uwezo wa Kushinda Hofu


Download audio file

 Imani ya kweli ndani ya Yesu ni jambo jema.  Jema kabisa.  Kwa hiyo, kwa imani mtu anapiga hatua kwa kutumia vipawa na vipaji aliyopewa na Mungu kwa nia njema.

Ni jambo jema kabisa kuwa na imani ya kweli kwa Mungu; imani inayoendelea kupitia hali zote.  Jana tuligundua kwamba moto ule mdogo unaweza kuchochewa uwe mkubwa sana kadiri mtu atazoeza vipawa na vipaji alivyopewa na Mungu kwa ajili ya utukufu wake.  Na ndivyo ilivyoandikwa katika Neno la Mungu:

2 Timotheo 1:5-6  Nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.  Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. 

Lakini bila shaka, wakati mtu anaanza kupiga hatua ya imani kwa kutumia vipawa vyake na kuwabariki wengine kwavyo na kuliletea utukufu jina la Yesu … mara moja atakutana na vipingamizi – vya kiroho na vya ulimwengu pia.  Hua inatokea kila mara.  Ndiyo maana Paulo anaendelea kuandika yafuatayo:  

2 Timotheo 1:7  Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.   

Ebu tafakari kidogo.  Wakati Shetani anakushambulia na nguvu zote za Jehanamu, Roho wa Mungu ni chanzo cha uwezo wako, upendo na kuwa na moyo wa kiasi.  Usiogope.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.