... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Zitupilie Mbali Dhambi Zako Zilizo Sirini

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 90:8 Umeyaweka maovu yetu mbele zako, siri zetu katika mwanga wa uso wako.

Listen to the radio broadcast of

Zitupilie Mbali Dhambi Zako Zilizo Sirini


Download audio file

Kupitia miaka isiyo michache, tumeshuhudia, wewe na mimi, viongozi wa Kikristo wasio wachache huanguka dhambini.  Anguko lao hao wote limeanzia sirini, katika dhambi iliyofichwa.  Matukio hayo yanaweza kutuletea somo ambalo linaweza kutufundisha na kutuokoa tusianguke kama wao.

Kama unafanya jambo ambalo lakupasa kulificha watu wengine, kumficha mke wako au mme wako, rafiki zako, watoto wako … inabidi kulichunguza kwa makini.  Kwa sababu karibu mara zote jambo lile linahusisha dhambi fulani. 

Hata kama watu wengine hawaoni kinachoendelea, kuna Mmoja anakiona.  Sikiliza Musa akiongea na Mungu: 

Zaburi 90:8  Umeyaweka maovu yetu mbele zako, siri zetu katika mwanga wa uso wako. 

Rafiki yangu, ujue kwamba ikiwa hivi karibuni au hata baadaye, lazima Mungu abainishe dhambi za siri na kuziweka nuruni.  Hii inaweza ikatokea katika maisha haya kama ilivyowatokea viongozi wale walioangukua ambao tumewataja hapo juu.  Ni huzuni kubwa lakini afadhali iwe hivyo ili mtu awe na fursa kuiacha dhambi ile na kutubu na kusamehewa na Mungu. 

Kilicho kibaya zaidi kabisa ni kwamba dhambi ile iliyofichwa kubainika siku ile ya hukumu wakati hakuna tena nafasi ya kutubu. 

Charles Spurgeon aliwahi kusema hivi:  “Bwana, utuepushe na watu ambao ni kama malaika katika umma, watakatifu kanisani lakini nyumbani ni kama mapepo wachafu.” 

Ninataka kukupa changamoto leo.  Uwe wazi ukijikagua.  Je!  Kuna dhambi iliyofichwa maishani mwako?  Je!  Umekumbatia giza hiyo ya kishetani sirini ukiwa unajionyesha kuwa malaika wa nuru machoni pa watu? 

Kama ipo, basi uwe na moyo wa kujituma.  Iweke nuruni mwa Mungu.  Uitatue ukiwa mbele zake.  Kwa sababu ameyaweka maovu yetu mbele zake, siri zetu katika mwanga wa uso wake.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.