... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ahadi ya Krismasi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Samweli 7:12-16 Nawe siku zako zitakapotimia, ukalala na baba zako, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, nami nitaufanya imara ufalme wake. Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakifanya imara milele. Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu; lakini fadhili zangu hazitamwondoka, kama vile nilivyomwondolea Sauli, niliyemwondoa mbele yako. Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitshwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitafanywa imara milele.

Listen to the radio broadcast of

Ahadi ya Krismasi

Download audio file

Ujio wa Yesu hapa duniani ulikuwa tofauti kabisa na namna sisi tutakavyosherehekea Krismas juma lijalo. Ujio wake ulikuwa na mafumbo na siri.

Kwa muda wa miaka zaidi ya elfu moja sasa, Mungu aliwaambia watu wake teule, Israel, habari ya Mwokozi ambaye angewatumia siku moja. Manabii walifululiza utabiri unaohusu ujio wake. Lakini kwasababu watu walitazamia Mfalme shujaa mpiganaji ambaye angewaokoa na himaya ya Warumi (kitu ambacho Mungu kamwe hakukusudia) hawakuelewa lolote. 

Sikiliza unabii mojawapo uliotabiriwa na nabii Nathani akimwambia Mfalme Daudi miaka elfu moja kabla Yesu hajazaliwa: 

2 Samweli 7:12-16  Nawe siku zako zitakapotimia, ukalala na baba zako, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, nami nitaufanya imara ufalme wake.  Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakifanya imara milele. Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu; lakini fadhili zangu hazitamwondoka, kama vile nilivyomwondolea Sauli, niliyemwondoa mbele yako.  Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitshwa milele mbele yako.  Nacho kiti chako kitafanywa imara milele. 

Ebu angalia alivyoongea kuhusu dhambi, mapigo na adhabu?  Kawaida, huwa haitokei juu ya wafalme! Lakini kumbe!  Mungu hakumtuma Yesu kuokoa watu wake na mazingira yao magumu ya Warumi. Alimtuma Yesu kuwaokoa na dhambi zao – hakutuokoa sisi na dhambi zetu pia – kwa kukubali kubeba adhabu tulizostahili kuzipata.  Hili ndilo lengo la Mungu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.