... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hakikisha Ukweli wa Mambo Kabla ya Kutupa Mawe

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Kumbukumbu 17:6 Huyo atakayeuawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili, au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja.

Listen to the radio broadcast of

Hakikisha Ukweli wa Mambo Kabla ya Kutupa Mawe


Download audio file

Kuna utofauti mkubwa kati ya tendo lililotendeka kweli na maoni tu ya mtu.  Hayo tunayajua, lakini siku hizi ni kama watu hawafuati tena kanuni hiyo. Yaani siku hizi hata kama mtu ukiwa na maoni ye uhakika lakini ukimkwanza mtu hata kidogo basi utakuwa umekosea!

Juzi niliona katuni iliyonichekesha sana kwenye TV, yaani kulikuwa na mchezo wa watu watatu wakishindana halafu kuna simamizi mmoja, kila mchezaji alikuwa na kengele ya kubonyeza wakati wa kujibu swali, Julie alitoa jibu sahihi kwa mdomo lakini Petro alifinya kengele yake kwa sauti, Sasa msimamizi alimwambia “Julie, pole, umetamka jibu sahihi lakini ulipaswa ufinye kengele hivyo Petro ndiye aliyepatia na ameshinda

Inachekesha, lakini inahuzunisha pia kwasababu ndivyo mambo yanavyokwenda siku hizi. Ni kama yule anayepiga kelele zaidi ndiye ashindaye, hususani pale mambo yaliyo dhairi yanapokwenda kinyume na maoni ya mtu. 

Katika Agano la Kale, hukumu ya kifo ilikuwepo kama ilivyoleo kwenye baadhi na nchi duniani. Haya ndiyo asemayo kwenye sheria ya Waebrania kuhusu kuthibitisha na kuhakikisha yaliyotendeka kweli kweli: 

Kumbukumbu 17:6  Huyo atakayeuawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili, au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja. 

Kwanini haja ya mashahidi wawili au watatu!?  Kanuni ni kutafuta ukweli wa mambo badala ya kukubali mashtaka ya ajabu ajabu ya upande mmoja tu. 

Ni kweli, kila mtu ana haki ya kuwa na maoni yake na ni kawaida watu wawili kutazama tukio moja kwa mtazamo tofauti.  Lakini ni jambo baya sana kumsigizia mtu na kumshitaki kwa uongo, kwa kutumia udanganyifu na kupiga kelele zaidi ya wengine.  Hakikisha ukweli wa mambo yaliyotokea kabla ya kutupa mawe.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.