... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hatia na Fadhaa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Timotheo 1:7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

Listen to the radio broadcast of

Hatia na Fadhaa


Download audio file

Kuendela kujisikia kwamba una hatia kwa sababu ya makosa uliyoyafanya zamani pamoja na kuwa na fadhaa kwa kufikiria itakavyokuwa mbeleni, ni kama pande mbili za sarafu moja. Na kwa watu wengi, adui hao wawili wanawakosesha amani rohoni na kuathiri hata uhai wao.

Kama unamwamini Yesu kweli kweli na kumkabidhi maisha yako mikononi mwake, na kukusudia kumwishia yeye, basi kuna kitu kimoja unaweza kuwa na uhakika nacho:  ni hiki, dhambi zako zote na makosa yako yote uliyoyafanya zamani vimesamehewa kabisa kabisa.  Swali linabaki kwako, je! Na wewe umejisamehe? 

Kuna jambo lingine pia ambalo unaweza kuwa na uhakia nalo. Kila dakika ya maisha yako iko mikononi mwake; kila hatua unayopiga, yuko sambamba.  Kamwe huwezi kuwa peke yako. Hawezi kukusahau. Sasa je!, unaishi kana kwamba hayo yote ni kweli? 

nisikilize vizuri, hata mtu akiendelea kujisikia kuwa na hatia, hali hiyo haiwezi kubadilisha yaliyopita. Pia fadhaa nyingi hazitabadilisha mambo yanayokuja.  Ni katika Yesu tu, mtu anaweza kupata msamaha kamili.  Ni katika yeye tu, mtu anaweza kujisikia salama na kutulia akifikiri siku zijazo.

Halafu ili hayo yote yatende kazi ndani yako, amekuachia Roho wake Mtakatifu kukaa ndani yako, akubariki na kukuponya: 

2 Timotheo 1:7  Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. 

Kama kweli unamwamini Yesu, basi unauwezo wake, unao upendo wake.  Pia umeshapewa hekima zote na uwezo wa kujithibiti ili uwekwe huru na hatia na fadhaa ambazo vinakuibia uzima tele Yesu aliyekupa pale alipokufa na kufufuka tena. Huu ndio ukweli kabisa! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.