... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kumlaumu Shetani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yakobo 1:13-16 Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa mauti. Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike.

Listen to the radio broadcast of

Kumlaumu Shetani


Download audio file

Huwa haipendezi pale mtu anaposhindwa na jaribu,  Sasa nani wakulaumiwa?  Je!  Ni sisi wenyewe?  Lakini wengine watasema ni Shetani.  Wengine wanauliza, kwa nini Mungu alimruhusu Shetani anijaribu?

Swala la kutupiana lawama huwa ni ishara ya mtu kushindwa na jaribu.

Yakobo 1:13-16  Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.  Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa nakudanganywa.  Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa mauti.  Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike. 

Tunyoshe mambo kwanza.  kwanza, tujue kwamba Si asili ya Mungu kutujaribu, kwa hiyo yeye mwenyewe hawezi kutujaribu.  Na hata kama Shetani anahusika mara kwa mara, katika mistari hii Mungu anaweka lawama zote juu yetu sisi wenyewe. 

Ni kwamba, mtu unatamani kitu ambacho huna – hii ndiyo cheche ya matamanio.  Kadiri unavyoendelea kufikiria kile kitu, ndivyo unavyozidi kushawishika na kuvutwa nacho.  Cheche za tamaa zikichochewa na fikra huwa zinageuka na kuwa dhambi.  Halafu kadiri unavyotenda dhambi ndivyo unavyozidi kufuata njia iendayo kwenye mauti ya milele. 

Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike.  Kuna wakati  si Shetani anakujaribu, bali ni maamuzi yako wewe mwenyewe.  Kwahiyo, jaribu kudokeza tamanio linalokuongoza kila wakati kutenda dhambi.  Lipeleke na uliache msalabani. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.