... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kutupa Mawe, Kuosha Miguu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 13:1-5 Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo. Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, moyo wa kumsaliti; Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu, aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni. Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.

Listen to the radio broadcast of

Kutupa Mawe, Kuosha Miguu

Download audio file

Ni vigumu sana kupenda watu wasikupenda, si kweli?  Kikawaida huwa tunataka kuwaumiza kama walivyotufanyia sisi.  Ndio maana kuna migogoro mingi duniani.

Nakumbuka nilipokuwa mtoto nilipigana na baadhi ya wanafunzi wenzangu hadi tukarushiana mawe.  Hayo sion maadili kabisa.  Lakini kinachohuzunisha zaidi ni kuona baadhi ya watu wanaendelea na tabia hiyo na huku wameshakuwa watu wazima. Hata kama hawatupiani mawe kama mawe, bado wanagombana kila wakati hawaelewani kwa kutupiana maneno makali. Lakini tumwangalie Yesu sasa: 

Yohana 13:1-5  Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo.  Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, moyo wa kumsaliti; Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu, aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni.  Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga. 

Kinachonitikisa hadi kiini cha moyo wangu katika habari hiyo ni kwamba, Yesu alimtawadha Yuda miguu na huku akijua kanisa kuwa atamsaliti. 

Kumbukumbu: Ni vigumu kutupa mawe wakati uko bize kwa kutawadha miguu watu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.