... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usitapanye Uhuru Wako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wagalatia 5:1 Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.

Listen to the radio broadcast of

Usitapanye Uhuru Wako


Download audio file

Kuna jambo moja bado linanisumbua kuhusu wazazi wangu, ni kwamba, yale yote waliyojaribu kunifundisha nikiwa kijana mwenye dharau, hatimaye nimekuja kugundua kumbe sahihi kabisa!

Kuna mambo wazazi wetu walijitahidi sana kuyasisitiza mara kwa mara tulipokuwa vijana lakini hatukuwaelewa; tukadharau na kugeuzageuza macho huku tukifikiri mioyoni mwetu na kuwaona, “Hawajui lolote!” 

Lakini kule kufundishwa kuwa na adabu wakati wa chakula na kusaidia nyumbani bila kuambiwa …  ninani alifikiri kwamba ingeleta faida maishani mwetu. Ninani angefikiria?  Sio mimi! 

Mithali 13:1  Mwana mwenye hekima husikiliza mausia ya babaye;  bali mwenye dharau hasikilizi maonyo

Mimi sikuwahi  kuwa motto mwenye hekima, nilikuwa mzito sana wa kufundishwa. Lakini kadiri miaka ilivyokuwa inazidi kwenda nilifikia maamuzi ya kusema kwamba mtu anajifunza haraka masomo mbalimbali ya maisha na hapo ndipo utakapokuwa na hekima na maisha yako yatakuwa bora. 

Wiki lililopita tuliongea kuhusu namna inavyotupasa kupokea ushauri; na leo ilinibidi nirudie mada hiyo, kwasababu kusema ukweli, kukubali kukosolewa na kurudiwa … sio jambo rahisi kwa wengi wetu, au si sio? 

Mstari huu unatuonyesha wazi kwamba, hekima na kiburi haviendani, yaani ni mambo mawili tofauti kabisa. 

Mwana mwenye hekima husikiliza mausia ya babaye;  bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.  

Moyo wenye hekimu uko wazi daima, Moyo wa dharau na kiburi daima haviko wazi. Maisha yatakuwa bora pale mtu atakapokubali kujifunza, kurudiwa na kuwekwa sawa.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.