... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Yaliyo Haki na ya Kweli

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 33:4,5 Kwa kuwa neno la BWANA lina adili, na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu. Huzipenda haki na hukumu, nchi imejaa fadhili za BWANA.

Listen to the radio broadcast of

Yaliyo Haki na ya Kweli


Download audio file

Siku hizi ni vigumu kupambanua na kujua “ukweli” uko wapi.  Taarifa zimefurika mno na nyingi hazijatoka kwenye moyo mweupe.

Bila kuegamia upande wowote, kuna kitu kimoja kinahusu janga la CORONA ambacho kinatatanisha mno. Ni swala la chanjo na mabishano kati ya wale wanaotetea chanjo na wanaoikataa (bila shaka nimetonesha watu baadhi,lakini mniwie radhi.) 

Kinachonitatanisha ni kuona namna ambavyo watu wanaofanya utafiti mmoja kupishana katika majibu.

Mgogoro huo unatokana na mtazamo wa mtu mwenye nia na makusudi ya serekali, mashirika, ma-kampuni na wasemaji mbalimbali na kadhalika.  Na ni kweli, mara nyingi makusudi baadhi siyo safi.

Na ndivyo ilivyo wakati watu wanakosoa habari za Mungu, kama wanavyozidi kufanya siku hizi wakipotosha wengi.  Motisha yao haitokani na moyo mweupe.  Kwahiyo, ukijisikia unataka kupotoshwa na uvamizi wa wapinzani wakijaribu kukufanya utilie mashaka Neno la Mungu, uelewe yafuatayo: 

Zaburi 33:4,5  Kwa kuwa neno la BWANA lina adili, na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.  Huzipenda haki na hukumu, nchi imejaa fadhili za BWANA. 

Tunaweza kuwa na uhakika kwamba Neno la Mungu ni adili, na tunaweza kumtegemea kwa sababu motisha yake inatokana na moyo mweupe kabisa.   

Huzipenda haki na hukumu, nchi imejaa fadhili za BWANA.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.