... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kufanya Makosa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 37:23,24 Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA, naye aipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, BWANA humshika mkono na kumtegemeza.

Listen to the radio broadcast of

Kufanya Makosa


Download audio file

Kinachosumbua zaidi maishani ni pale mtu anapodhamiria kutenda haki, lakini kwa njia moja au nyingine hafikii lengo lake.  Au labda ni mimi tu peke yangu?  Hapana, sidhani.  Tunaanza vizuri tukiwa na makusudi mema lakini hatimaye tunafeli.

Hata ukiita kule kushindwa kuwa dhambi au kutereza, namna tunavyoeleza haina umuhimu zaidi ya matokeo yake. Mimi binafsi nina shauku ya kumfuata Yesu. Shauku kubwa kweli.  Naamini au ninaomba kwamba na wewe uwe nayo pia.  

Mtu akielewa yote Yesu aliyotutendea pale alipokufa msalabani na kulipa gharama iliyodaiwa na haki ya Mungu kwa ajili ya dhambi zetu, ndipo atazidi kuwa na nia ya kumheshimu, kumfuata, kumtumkia na kumtii. 

Halafu tuna uhakika kabisa kutokana na Maandiko kwamba Mungu anapenda kuona kwamba mioyo yetu ina mwelekeo sahihi kama huo.  Sasa tukijikwaa inakuaje?  Tukimkosea tunafanyaje? 

Zaburi 37:23,24  Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA, naye aipenda njia yake.  Ajapojikwaa hataanguka chini, BWANA humshika mkono na kumtegemeza. 

Kweli Bwana anatuonyesha namna tunavyopaswa kuishi. Anapendeza kweli akiona kwamba tunaishi hivyo.  Angalia tena maneno ya mstari wa 24: 

Ajapojikwaa hataanguka chini, BWANA humshika mkono na kumtegemeza.  

Yupo pale pale pembeni yetu akiwa tayari kututegemeza tukijikwaa ili tusianguke.  Hii ni habari njema kabisa, si kweli? 

Mimi naona kwamba, kosa linalokudunisha na kukufanya uitegemee neema ya Mungu ni bora kuliko kufanikisha jambo lingelokupa kiburi. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.