... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuishi Katika Ushindi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorinto 10:13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweza kustahimili.

Listen to the radio broadcast of

Kuishi Katika Ushindi


Download audio file

wanadamu wanapozidi kuwa na matengano kwenye masuala ya jamii, siasa na dini, pale majadiliano yanapokuwa ni ugomvi mtupu, na ule utengano ukizidi kupanuka, ni rahisi sisi kuzidi kuwa wakosoaji tu.

Ninachokisema ni kweli, sindiyo?  Hususani ukishiriki kwenye vyombo vya kijamii mtandaoni. Ni rahisi sana siku hizi kuwa mkosoaji.  Tunajenga makabila yanayolenga mawazo na mitazamo na dini tofauti tofauti na tunafikiri kwamba ni wajibu wetu kutetea vya kwetu na kujihami na wale tunaowaona ni adui.  Lakini Hali hii ndiyo lengo la maisha? 

Mwanafalsafa Mgiriki aitwaye Aristotle aliwahi kusema hivi:  “Namhesabu kuwa jasiri mtu anawezaye kuthibiti matamanio yake mwenyewe kuliko yule anayeshinda maadui; kwa sababu ushindi mgumu zaidi ni kushinda tamaa zetu binafsi.” 

Ni kweli kabisa!  Kuthibiti tamaa zetu – hususani kuthibiti ulimi – kwa kweli ni kazi ngumu ambayo siku zingine inaonekana kwamba haiwezekani.  Lakini tumejaliwa kuwa na msaidizi wa kuthibiti tamaa zetu.  Kwasababu, yule aliyekusudia kwa moyo wake wote kumfuata Yesu kwa karibu, kuna uwezo mwingi kuliko tunavyouhitaji unaotusaidia kushinda yote yaliyomo ndani mwetu ambayo tunatambua kuwa ni maovu. 

1 Wakorinto 10:13  Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweza kustahimili. 

Wewe na mimi, hatuwezi kuwabadilisha watu walioko huko, hata tujitahidije kuhojiana nao.  Lakini tunaweza kujiangalia kwenye kioo, bila kujidanganya na kujibadilisha tabia, jitihada ambazo hatuzifanyi peke yetu kwa sababu Mungu yuko pamoja nasi katika kazi hiyo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.