... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kumpiga Mtu Kwa Mawe

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 10:30,31 Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige. Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe?

Listen to the radio broadcast of

Kumpiga Mtu Kwa Mawe


Download audio file

Kuwapiga Wakristo kwa mawe siku hizi ni kama kawaida. Kwa sehemu ni kwasababu ya unafiki uliopo kati yetu. Sawa,  hakuna anayependa unafki.  Lakini kuna sababu zingine zinawasababisha kufanya hivyo.

Kwa wale wengi ambao hawamwamini Yesu, imani yetu kwake inawakwaza sana. Ninawaelewa. Kabla sijawa Mkristo, acha nikwambie, yale wale Wakristo waliyoyasema na kuyafanya, hata matendo mema (hususani matendo mema!) yalinikwaza mno. 

Niliwachukia, niliwatesa, niliwatupia mawe, Sasa mtu akitafakari kidogo, lazima ajiulize … kwanini niliwatendea hivyo? 

Kwa mafupi, ni kwa sababu wema wao ulimulika kwenye giza la moyo wangu; giza iliyokuwa imeenea kote katika maisha yangu. Na kama kansa, ilinishinda mimi peke yangu kuvunja pingu zake ili niwe huru. Kwahiyo niliitetea na kuikumbatia kwa nguvu zangu zote. 

Na hali hiyo ndiyo iliyokuwepo katika habari tunayoisoma katika Injili ya Yohana: 

Yohana 10:30,31  Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige.  Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? 

Kusema ukweli, walimwua! Tunafahamu kwamba hakuna anayependwa kutupiwa mawe kwasababu ya imani yake ndani ya Yesu, lakini yeye alitabiri kwamba itatokea. Hakuna anayependa kusulubiwa kama Yesu, lakini ametuita tuchukue kila mtu msalaba wake na kumfuata. Usishangae wakati watu wanakutupia mawe.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.