... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mungu Hawezi Kukupungukia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 3:9,10 Mheshimu BWANA kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.

Listen to the radio broadcast of

Mungu Hawezi Kukupungukia


Download audio file

Kuna swala la muhimu tunapaswa kulitafakari mwanzoni wa mwaka huu.  Ni kupanga bajeti, hususani tukiona namna gharama za kila kitu zinapanda na kubana uchumi wetu.  Je! utasimamiaje mapato yako mwaka huu?

Kuna watu baadhi hawaongozwi na bajeti yoyote, wakitumia hela kiholela kama kubahatisha tu. tajiri mkubwa labda angeweza kufanya hivyo kwa muda fulani, lakini kwa sisi watu wa kawaida, sio busara. 

Kwahiyo, kadiri mtu anavyozidi kuona bei zinapanda, mfano, ada ya nyumba, pesa kupoteza thamani yake n.k., kweli inaleta wasiwasi na mtu atasema moyoni mwake … Lazima ni punguze matumizi. 

Sasa, watu wengi wakianza kubana matumizi, la kwanza wanapunguza sehemu hasa wanazotoa kuwasaidia maskini na kuwezesha kazi ya Mungu.  Ni rahisi kuanzia hapo kwasababu inaonekana kwamba haitadhuru hali ya maisha yao.  Unielewe vizuri, Mungu hatazamii utoe kitu ambacho hauna. Lakini pia, hatazamii sisi watu wake kujikinga mara moja kwa kupunguza matoleo yetu. 

Kwa hiyo, ukichunguza sasa bajeti ya familia yako, acha nikupe neno la hekima ya Mungu liongoze fikra zako: 

Mithali 3:9,10  Mheshimu BWANA kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote.  Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, na mashinikizo yako yatafurika divai mpya. 

Sijaona kanuni bora kwa kuniongoza katika swala la uchumi kuliko hili.  Hata kama tumepitia vipindi vya kutisha kwenye huduma zetu zinazoendeshwa kwa imani tu.

wewe na mimi tunajitolea na kutoa kwa ukarimu kwa ajili ya kazi ya Mungu, kamwe hatatupungukia.  Mungu anawaheshimu wanaomheshimu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.