... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uwazi Katika Hisia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 9:4-6 Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, Njoo ule mkate wangu, ukanywe divai niliyoichanganya. Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, mkaende katika njia ya ufahamu.

Listen to the radio broadcast of

Uwazi Katika Hisia


Download audio file

Wengiwetu tuna upungufu huu:  tunashindwa kusoma hisia za watu wengine – kabla ya kutamka au kutenda.  Lakini pia, tunashindwa kuelewa kitu kingine cha muhimu zaidi.

Hicho kitu kingine ni kuelewa hali ya hisia zetu kabla hatujatamka au kutenda.  Labda umesononeka, kwahiyo, badala ya kumshukuru mtu, unamtendea kana kwamba yeye ni kitu wala si mwanadamu.  Au labda umekasirika, kwa hiyo unatamka kwa haraka bila kuelewa kama una hasira, na maneno uliyoyasema huwezi kuyarudisha tena. 

Yaani mazingira ya hisia zetu kwa ujumla hayako wazi, bali ni yenye giza tu, si kweli?  Sasa namna tunavyotambua hisia zetu na za watu wengine na jinsi tunavyoitikia kufuatana na uelewa wetu unaleta mtikisiko mkubwa katika hali ya maisha tunayoishi.  Basi leo, hekima – hekima ya Mungu – inatupigia kelele kwa kutuita. 

Mithali 9:4-6  Kila aliye mjinga na aingie humu.  Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, Njoo ule mkate wangu, ukanywe divai niliyoichanganya.  Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, mkaende katika njia ya ufahamu. 

Jibu linaloweza kutuletea uwazi kwa kuelewa hisia mbali mblai ni kula na kunywa hekima ya Mungu.  Halafu Neno lake – yaani Biblia – imejaa hekima kabisa. Mna utambuzi na habari ya uwezo wa Roho Mtakatifu tunavyohitaji kutafakari namna tunavyohisi kwa ndani kabla hatujatamka au kutenda. 

Ni aina ya hekima tunayohitaji ili tuweze kuelewa mazingira ya yule mwingine tunayokutana naye.  Kwahiyo … acheni ujinga, mkaishi, mkaende katika njia ya ufahamu.  

Mungu amekuitia hayo.  Amekupa ofa maalumu kukusaidia katika tatizo hilo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.