... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uwe na Moyo Mkuu Kipindi Hiki Chenye Wasiwasi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mhubiri 7:14 Siku ya kufanikiwa ufurahi, na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake.

Listen to the radio broadcast of

Uwe na Moyo Mkuu Kipindi Hiki Chenye Wasiwasi


Download audio file

Haijalishi tunajikuta katika mazingira gani muda huu huu, yakiwa mema au mabaya, lazima yatagusa mtazamo wetu katika maisha haya.

Ni dhairi kwamba mazingira mazuri yanatuinua kama vile mazingira mabaya yanavyotusononesha.  Hisia zetu hua zina mwitikio wa haraka dhidi ya hali ya mazingira tuliyomo.  Ni nani anayependa kupambana na mabaya? 

Baada ya kusema haya, jua kwamba wakati mabaya yanakukabili, yakikuvamia moja kwa moja au yakija chini chini bila kutazamamisha, inabidi ufikirie kidogo.  Ni yapi yaliyomo maishani mwako sasa hivi ambayo usingeyachagua?  Ndani yako unahisi nini? 

Ni kweli kwamba kushuka na kupanda ni kawaida katika maisha ya mwanadamu, ila mwisho wa siku, Mungu hakutuumbia kutikiswa hivyo daima.  Hakuna apendaye kuishi daima katika misukosuko kama hiyo.  Kwa hiyo … 

Mhubiri 7:14  Siku ya kufanikiwa ufurahi, na siku ya mabaya ufikiri.  Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake. 

Ukweli ni kwamba Mungu bado anatawala juu ya mazingira yote ambayo tunakabiliana nayo … leo, kesho, kesho kutwa.  Lazima tufurahie siku ya kufanikiwa, wakati Mungu anatukirimia baraka.  Ni jambo jema kabisa. 

Lakini wakati maisha yanatuwia vigumu, kumbuka hili:  kwamba siku mbaya na zenyewe zinatoka kwa mkono wa Bwana, naye ni wa kuaminiwa kabisa.  Kwa hiyo, ukikabiliana na kipindi kigumu, uwe na moyo mkuu hata katikati ya wasiwasi, kwa sababu Mungu wako anastahili kuaminiwa. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.