... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Amani Bora Sana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 14:27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.

Listen to the radio broadcast of

Amani Bora Sana


Download audio file

Kuna wakati maisha yetu ni kama mtu amefuliwa ndani ya mashine ya kufua nguo na hatimaye kuwekwa kwenye mashine inayokausha  huku akizungushwa zungushwa hadi nguvu zake zote zinaisha.

Wanaokana Mungu wanaushtaki Ukristo kwamba ni kwa ajili ya wanyonge tu; ni gongo la kutembelea viwete. Lakini si watu wanaoshindwa na maisha ambao wanaweza kupatwa ghafla na msiba; wala si wanyonge tu ndio wanaweza kupinduliwa na watu wengine au mazingira yanayoenda hovyo mpaka nguvu za mwili na za hisia na za kiroho ziishe kabisa.  Huwa inaweza kuwapata na wenye nguvu, wenye akili, na watu wepesi pia. 

Sasa katikati ya misukosuko, kinachohitajika hasa ni amani.  Tuna hamu ya amani katikati ya uchovu na unyonge. 

Shida iliyopo ni pale mambo yanapokuwa magumu sana, wakati mwingine ni yale ambayo watu wenye nia njema wangesema au kutenda mamnbo yasiyo na nguvu kukufikia pale unapozama kwenye bahari iliyochafuka wala kutuliza mawimbi na kufanya maji yawe shwari. Amani yoyote inayotolewa na dunia ni ya muda mfupi tu.  Nafikiri umeshashuhudia hayo, sindiyo? 

Ni kwasababu hiyo hiyo Yesu – Mwana halisi wa Mungu aliyeteswa na kufa kwa ajili yako – ana la kusema kuhusu misukosuko iliyoko leo hii: 

Yohana 14:27  Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo.  Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. 

Halafu  pale Yesu anapotamkia amani moyoni mwako, inakuja ikitegemezwa na uweza wa Mungu mwenyewe. Nisikilize. Yesu anaweza kukuletea amani inayohusu yaliyopita maishani mwako, na yaliyopo sasa na yale unayotumaini mbeleni.  Yesu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.