... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kilio cha Kuomba Msaada

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 61:1-4 Ee Mungu, ukisikie kilio changu, uyasikilize maombi yangu. Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, ngome yenye nguvu adui asinipate. Nitakaa katika hema yako milele, nitaikimbilia sitara ya mbawa zako.

Listen to the radio broadcast of

Kilio cha Kuomba Msaada


Download audio file

Kazi mojawapo ya mzazi ni kulinda watoto wake.  Na mimi kama mme, baba na sasa babu, ni wajibu ambao ninakubali kwa dhati kabisa.  Sasa kwa nini mtu angefikiri kwamba Mungu angekuwa tofauti katika swala hilo?

Juzi tuliongea habari ya maisha kuwa na mabonde na milima. matatizo tunayoyapata yanageuka kuwa msiba mkubwa.  Sikiliza maneno ya mtu aliyeniomba juzi nimkumbuke katika maombezi: 

Nimeshindwa kwenda kazini kwa sababu ya fadhaa na kukatishwa tamaa.  Ninahangaika kweli kiuchumi na yote ninayoyafanya yanafeli tu.  Nimeshindwa kukidhi mahitaji ya watoto wangu kwa ajili ya masomo; kununua rimu ya kartasi, sare na ada. 

Kawaida, matatizo hua yanatujia kwa njia mbali mbali, mengine makubwa, mengine ya wastani.  Kwa hiyo nilipenda leo tuchunguze zaidi kwa kutafiti tunafanyaje wakati tumefika chini kabisa na kujikuta tuna hali duni mno. 

Zaburi 61:1-4  Ee Mungu, ukisikie kilio changu, uyasikilize maombi yangu.  Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.  Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, ngome yenye nguvu adui asinipate.  Nitakaa katika hema yako milele, nitaikimbilia sitara ya mbawa zako. 

Mfalme Daudi aliyeandika dua lile, alikuwa mfalme mkubwa katika Israeli kuliko wote hadi pale mfalme mwingine wa aina tofauti kabisa aitwaye Yesu alionekana baada ya miaka elfu moja.  Lakini mfalme huu Daudi aliyekuwa hodari katika vita anamlilia Mungu akakiri … Nimezimia moyo! 

Halafu, rafiki yangu, acha nikwambie kwamba dua hilo, kama lilimfaa shujaa kama Daudi, basi itatufaa watu kama sisi, wewe na mimi.  Mungu wako ni mlinzi wako.  Upaze sauti ukamlilie kwa sababu yeye anawajibika sana na kazi hiyo ya kukulinda. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Receive the FRESH devotional daily.

Dive deeper into God’s Word and grow closer to Jesus.

I want to receive God's Word FRESH daily!